ear4u

Karibu katika Ear4U.

Pamoja kwa ajili ya kudumisha na kuboresha maisha ya siku za usoni.

Kulinda haki za binadamu na mazingira katika mkondo wa usambazaji wa kahawa ni muhimu kwetu. Kama kampuni za sekta ya kahawa, tumeungana pamoja chini ya mwavuli wa Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association). Pamoja tunajitahidi kufanikisha lengo la kuboresha zaidi mkondo wa usambazaji wa kahawa. Ili kufanikisha lengo hili, tunategemea msaada wako: Tafadhali tujulishe kuhusu masuala au malalamiko yanayoathiri kazi yetu.


Powerd oleh

 

Bekerjasama dengan

Ni muhimu na sawa kutujulisha kuhusu malalamiko yaliyopo.

Habari zote zinazowasilishwa zitachunguzwa kwa usiri na kwa undani. Kampuni huru ya GRAS (Global Risk Assessment Services) inatusaidia katika suala hili. Kadri unapotupatia habari kamili na ya kina, ndivyo tunaweza kuchunguza ombi lako haraka na kikamilifu. Kwa hivyo tunaomba: Ikiwa inawezekana, tupe maelezo kuhusu maswali yafuatayo: 
Nini kilichofanyika? Wakati gani? Wapi? Ripoti hiyo inahusu kampuni gani?

Ni nini kinachoweza kuripotiwa?

Tafadhali tujulishe kuhusu masuala ya hatari za haki za raia na mazingira kwenye mikondo yetu ya usambazaji. Ifuatayo ni mifano ya maoni na masuala unayoweza kuripoti:

Ajira ya Watoto

Ajira ya lazima na utumwa

Ukosefu wa usalama kazini

Ukiukaji wa haki na uhuru wa raia (k.m. uhuru wa kutangamana na haki ya kudai malipo mazuri)

Ubaguzi kazini

Mishahara isiyofaa

Uchafuzi wa mazingira

Ukiukaji wa haki za ardhi

Ukiukaji wa haki za binadamu na maofisa wa usalama katika mazingira ya kazi

Ni nini kinachoweza kuripotiwa?

Ahadi yetu: 
Hutatam-
bulishwa.

Fomu ya mtandaoni ya bila malipo

Wasilisha suala lako mtandaoni sasa hivi: HAPA.

  • Kiungo hicho kinakupeleka katika mfumo wa SpeakUp® wa Ear4U.
  • Baada ya kuingia, andika maelezo yako kwenye fomu ya mtandaoni.
  • Inachukua dakika chache tu kujaza fomu hiyo.
  • Unaweza pia kupakia hati (k.m. picha) ukipenda.
  • Nambari ya ripoti huwekwa kiotomatiki kwa suala lako ulilowasilisha. Unaweza kuitumia kuingia katika mfumo wa SpeakUp® wa Ear4U wakati wowote (HAPA) na uone jinsi uchakataji wa ripoti yako unavyoendelea.

Wasilisha suala lako mtandaoni sasa hivi: HAPA.

Laporkan secara online

Programu ya bila malipo

Je, ungependa kuwasilisha suala lako kupitia programu ya SpeakUp®?

  • Unaweza kupakua programu bila malipo, kwenye duka la "App Store" (kwa vifaa vya iPhone au iPad) au kwenye duka la “Google Play" (kwa simu zingine zote za mkononi na tableti).
  • Unaweza kuingia kwenye mfumo wa SpeakUp® wa Ear4U kupitia programu hiyo.
  • Baada ya kuingia, weka msimbo wa 103720 na uwasilishe habari yako kwa maandishi au kwa ujumbe wa sauti.
  • Unaweza pia kupakia hati (k.m. picha) ukipenda.

Silakan klik di sini:

Google Play App Store

Nambari ya Huduma ya dharura

Je, ungependa kuelezea suala lako kwa simu?

Tafadhali tumia nambari ya huduma ya dharura ya nchi unakopigia simu. Unapopiga simu, tafadhali taja msimbo ufuatao: 103720

Kenya
Nambari ya simu: +254 20 765 0957

Simu inatozwa gharama ya nchini ya kupiga simu kwa dakika.

Tanzania
Nambari ya simu: 0800 11 1020

Haulipishwi kwa kupiga simu hii.

Uganda
Nambari ya simu: +256 41 423 8162

Simu inatozwa gharama ya nchini ya kupiga simu kwa dakika.

Ethiopia
Nambari ya simu: 800 86 1919

Haulipishwi kwa kupiga simu hii.

Pakua orodha yenye nambari zote za simu kama faili ya pdf.

Pakua sasa

Ni nini kitakachofanyika kwa ripoti yangu?

1. Utapokea nambari ya ripoti ya binafsi.

Nambari ya ripoti itawekwa kiotomatiki kwenye ripoti yako ya siri. Tafadhali hifadhi nambari hiyo vizuri. Unaweza kuitumia kuingia katika mfumo wa SpeakUp® wa Ear4U wakati wowote (HAPA) na uone jinsi uchakataji wa ripoti yako unavyoendelea. Baada ya kuwasilisha ripoti yako, utapokea uthibitisho wa kiotomatiki wa kuwasilishwa.

2. Ikiwa inahitajika, tunaomba maelezo zaidi.

Ili tuweze kushughulikia ripoti yako haraka na kikamilifu, tunahitaji maelezo - ikiwa yapo - kwa maswali yafuatayo: Nini kilichofanyika? Wakati gani? Wapi? Ripoti hiyo inahusu kampuni gani? Ikiwa hatuna maelezo muhimu ambayo yatatusaidia kushughulikia ombi lako, kampuni huru ya GRAS inaweza kuwasiliana nawe kupitia mfumo wa siri wa SpeakUp®. Utaamua mwenyewe iwapo ungependa kutoa maelezo zaidi ya hiari kuhusu suala lako.

3. Tutakagua ripoti yako.

Maelezo yote yanayowasilishwa huchunguzwa kikamilifu na kwa undani. Hoja zifuatazo ni vigezo muhimu vya ukaguzi: Je, ripoti yako inahusu masuala ya hatari za haki za binadamu au mazingira? Je, mikondo ya usambazaji ya kampuni moja au zaidi, ambazo zinahusika katika Ear4U, imeathiriwa?

Tutawasiliana nawe ndani ya siku kumi za kazi baada ya kuwasilisha ripoti yako kuhusu kipindi ambacho uchunguzi unaweza kuchukua. Uchunguzi wa kwanza hufanywa na kampuni huru ya GRAS. Kisha suala lako litachunguzwa na mtu wa kuaminika kutoka kwenye kampuni ambayo mkondo wake wa usambazaji unahusika kwenye ripoti. Kampuni itaamua iwapo itachukua hatua na hatua ya kuchukuliwa ili kushughulikia ripoti yako ipasavyo.

 

4. Tutakujulisha kuhusu matokeo ya uchunguzi wetu.

Mfumo wa SpeakUp® utakupa maelezo kuhusu jinsi ripoti yako itakavyoshughulikiwa na iwapo hatua zitachukuliwa au hatua za ziada zitakazochukuliwa.

Ahadi yetu: Hutatambulishwa.

Tunazingatia zaidi ulinzi wa faragha yako. Tunawahakikishia watoboa siri wote faragha kamili na kutotambulishwa. Unaporipoti suala lako (kwa kutumia nambari ya huduma ya dharura, fomu ya mtandaoni au kupitia programu), hakuna maelezo ya binafsi yanayoombwa au kukusanywa wakati wowote. Ukipenda, unaweza pia kujitambulisha.

Asante kwa imani na msaada wako.

Ripoti yako inatusaidia kuboresha zaidi sekta ya kahawa.