Menghubungi dan mencetak

Mawasiliano
Msimamizi wa tovuti hii ni Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association). Muungano mkubwa zaidi wa kampuni za kahawa barani Ulaya.

Wanaohusika:
Mhariri:
Deutscher Kaffeeverband e.V.
Steinhöft 5-7
20459 Hamburg
nambari ya simu: +49 (0)40-3742361-0
info@kaffeeverband.de
Nambari ya kitambulisho cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT): DE 118721246
Nambari ya kitambulisho cha kodi: 17/449/00944

 

Bodi ya Wakurugenzi:
Bent B. Dietrich, Luc Van Gorp, Bernd Schopf, Dkt. Frank Strege

Afisa Mkuu Mtendaji:
Holger Preibisch

Mkurugenzi Mkuu:
Prof. Dkt. Johannes Hielscher, LL.M. (Stockholm)

Nambari kwenye Sajili ya Miungano:  
Nambari ya usajili VR 4043 
Sajili ya Miungano ya Hamburg 
Mahakama ya Eneo ya Hamburg 
Caffamacherreihe 20 
20335 Hamburg 

Chapa
Tovuti ya Deutscher Kaffeeverband e.V. ina viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti za watoa huduma wengine. Ukifuata viungo hivi, utaondoka kwenye kurasa za Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association), ambao hauwajibiki kwa maudhui ya kurasa hizi za nje na kwa hivyo hauna wajibu wowote kwa kurasa hizo.

Maelezo kuhusu utatuzi wa mgogoro mtandaoni kulingana na Kifungu cha 14 Aya ya 1 ODR-VO: 
Tume ya Ulaya (European Commission) ina mfumo wa utatuzi wa mgogoro mtandaoni (OS), ambao unaweza kuupata katika http://ec.europa.eu/consumers/odr/. Anwani yetu ya barua pepe ni: info@kaffeeverband.de

 

Maelezo kuhusu utatuzi wa mgogoro wa mteja kulingana na kifungu cha § 36 VSBG:
Hatutashiriki katika utaratibu wa utatuzi wa mgogoro mbele ya bodi ya maamuzi ya mgogoro wa mteja kulingana na Sheria ya Utatuzi wa Mgogoro wa Mteja (Consumer Dispute Settlement Act) na hatulazimishwi kufanya hivyo.

Perlindungan data

Mdhibiti
Mdhibiti wa ushughulikiaji wa data kulingana na Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (“GDPR, General Data Protection Regulation”) ni kampuni ya Deutsche Kaffeeverband e.V., Steinhöft 5-7, D-20459 Hamburg (inayorejelewa pia kwenye hati hii kama “sisi” au “nasi”).

Data ya Binafsi
Tunakusanya tu data ya binafsi ikiwa unatoa habari hii kwa hiari.

Haki zako
Una haki ya kuomba maelezo kuhusu data tuliyohifadhi kukuhusu na, ikiwa data hiyo si sahihi, kuomba kuisahihisha au, iwapo data isiyoruhusiwa imehifadhiwa, kufuta data hiyo. Pia, una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usimamizi. Katika jiji la Hamburg, yafuatayo ndio mamlaka ya usimamizi:

Mkuu wa Ulinzi wa Data na Uhuru wa Habari wa Hamburg (Hamburg Commissioner for Data Protection and Freedom of Information), Ludwig-Erhard-Str 22 (ghorofa ya 7), 20459 Hamburg, nambari ya simu: 040 42854-4040, faksi: 040 42854-4000, barua pepe: mailbox@datenschutz.hamburg.de

Maelezo ya mawasiliano ya ofisa wa ulinzi wa data katika Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association)

Steinhöft 5-7, 20459 Hamburg, nambari ya simu: 040 3742361-0, faksi: 040 3742361-11, barua pepe: info@kaffeeverband.de

Data ya kawaida
Unapotumia tovuti yetu, seva yetu ya wavuti kwa kawaida hairekodi anwani yako kamili ya IP na jina la kikoa cha kompyuta inayotumika. Seva hiyo imewekewa mipangilio kwa namna kwamba maelezo yanayohitajika kwa ajili ya kumtambulisha mtu hayarekodiwi kiotomatiki. Kwa hivyo, hakuna data ya binafsi au ya kumtambulisha mtu inayoweza kurekodiwa kwenye seva zetu.

Seva ya tovuti ya Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association) hairekodi data yoyote ambayo inaweza kuruhusu watumiaji kutambuliwa kibinafsi. Unaweza kutumia mfumo wa mtandaoni wa Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association) bila kutambulika au kwa kutumia jina bandia.

Faili ya kumbukumbu inaweza kufunguliwa kwa ajili ya uchanganuzi wa hitilafu katika tukio la matumizi mabaya au hitilafu za seva pekee. Anwani ya IP, anwani maalum ya ukurasa uliofungua, labda ukurasa uliotumia kufungua tovuti ya Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association) (chanzo cha kiungo), kitambulishi cha kivinjari kilichotumwa, na tarehe na wakati wa mfumo wa kufunguliwa kwa ukurasa vinaweza kurekodiwa. Data hii itafutwa mara moja baada ya hitilafu husika kusuluhishwa na itatumiwa tu kuchanganua hitilafu husika. Tovuti ya Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association) haiwezi kuhusisha data ya kumbukumbu na mtu binafsi.

Utathmini wa takwimu

Kufuatilia kupitia Google Analytics
Tovuti hii inatumia Google Analytics, huduma ya takwimu za wavuti inayotolewa na kampuni ya Google Inc. ("Google"). Google Analytics hutumia faili zinazojulikana kama "vidakuzi", faili za maandishi ambazo huhifadhiwa kwenye kompyuta yako na huwezesha uchanganuzi wa matumizi yako ya tovuti. Kwa hivyo tunafuata maslahi ya muundo unaozingatia mahitaji wa huduma yetu ya mtandaoni kulingana na Kifungu cha 6 Aya ya 1 lit f) GDPR. Maelezo yanayotengenezwa na vidakuzi kuhusu matumizi yako ya tovuti kwa kawaida hutumwa kwa seva ya Google nchini Marekani na kuhifadhiwa hapo. Ikiwa kipengele cha kutotambulisha anwani ya IP kimewashwa kwenye tovuti hii, anwani yako ya IP itafupishwa mapema na Google ndani ya nchi ambazo ni wanachama wa Muungano wa Ulaya (European Union) au katika nchi zingine zilizopewa kandarasi za Nchi Washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (European Economic Area). Anwani kamili ya IP itatumwa kwa seva ya Google nchini Marekani na kufupishwa hapo katika hali maalum pekee. Kwa niaba ya msimamizi wa tovuti hii, Google itatumia maelezo haya ili kutathmini matumizi yako ya tovuti, kutunga ripoti kuhusu shughuli ya tovuti na kutoa huduma nyingine zinazohusiana na shughuli ya tovuti na matumizi ya intaneti kwa msimamizi wa tovuti. Anwani ya IP inayotumwa na kivinjari chako kama sehemu ya Google Analytics haitaunganishwa na data nyingine ya Google. Unaweza kuzuia kuhifadhiwa kwa vidakuzi kupitia mipangilio ya kivinjari chako; hata hivyo, tungependa kukueleza kwamba ukizuia vidakuzi, hutaweza kutumia vipengele vyote vya tovuti hii kikamilifu. Unaweza pia kuzuia Google isikusanye data iliyotengenezwa na vidakuzi na inayohusiana na matumizi yako ya tovuti (ikijumuisha anwani yako ya IP) na data hii kutochakatwa na Google kwa kubofya kiungo kifuatacho (http:// tools.google.com/dlpage/gaoptout?hl=de) na usakinishe programu-jalizi ya kivinjari inayopatikana.

Viungo vya tovuti zingineIkiwa tovuti ya nje imefunguliwa na tovuti ya Muungano wa Kampuni za Kahawa za Ujerumani (German Coffee Association) (kiungo cha nje), mtoa huduma wa nje anaweza kupokea maelezo kutoka kwenye kivinjari cha mtumiaji kilichotumiwa kwenye tovuti yetu. Mtoa huduma wa nje pekee ndiye anawajibika kwa data hii.